YANGA SASA USO KWA USO NA AL AHLY APRILI 9
Na Prince Hoza
Hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc itakutana na National Al Ahly ya Misri katika hatua ya kuelekea 16 bora.
Yanga imetinga raundi ya pili baada ya kuitoa mashindanoni jana APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, Yanga ilishinda mchezo wa kwanza ugenini mabao 2-1 na kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam jana.
Al Ahly nao walilazimisha sare ya ugenini dhidi ya Reacreative Libolo ya Angola ya 0-0 kisha kushinda 1-0 mjini Cairo, kwa matokeo hayo sasa Yanga itachuana na Al Ahly mchezo wa kwanza ukipangwa kuanzia jijini Dar es Salaam na wiki moja baadaye zitarudiana Misri.
Yanga ina kumbukumbu nzuri ya kushinda 1-0 jijini Dar es Salaam goli likifungwa na nahodha wake Nadir Haroub 'Cannavaro', ila ikafungwa 1-0 ziliporudiana Alexandria.
Yanga iliondoshwa kwa matuta 4-3 na hata hivyo Yanga yenyewe ilijilaumu baada ya kukosa penalti ya mwisho ambayo ingewapa ushindi