SIMBA YAHOFIA HUJUMA TANGA, YAAPA KUIUA COASTAL LEO

Na Salum Fikiri Jr,, Tanga

Wakati kikosi cha Simba kikiwasili juzi mjini Tanga na kufanya mazoezi yake katika uwanja wa Mkwakwani, kimehofia hujuma baada ya kuwapiga stop mashabiki waliokuwa wakija kuitazama.

Kikosi hicho kiliendelea kufanya mazoezi pasipo mashabiki na mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuuliza kulikoni muwazuie mashabiki wakajibu kuwa wanahofia hujuma.

Tanga kumekuwa na hujuma sana na hasa zinapokwenda kucheza Simba au Yanga, Simba leo jioni inakutana na Coastal Union mchezo wa ligi kuu bara.

Endapo Simba itashinda mchezo itakuwa inazidi kuziacha nyuma Yanga na Azam, hadi sasa Simba ina pointi 54 lakini imecheza mechi 23 tofauti na wenzao Yanga na Azam wenye 50 ambao wamecheza mechi 21.

Wakati Simba ikihofia hujuma za Coastal lakini kocha wa timu hiyo Jackson Mayanja amejinasibu kuchomoza na ushindi, Coastal ikituamia uwanja wa nyumbani imekuwa na bahati nzuri kwani imewahi kuzichapa Yanga 2-0 na Azam 1-0, Ngoja tuone

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA