KIIZA, LYANGA WAIPELEKA SIMBA JIRANI NA UBINGWA
Na Salum Fikiri Jr, Tanga
Washambuliaji Hamisi Kiiza "Diego" na Danny Lyanga jioni ya leo wameiwezesha Simba Sc kuchanja mbuga na kukaribia kabisa ubingwa wa bara baada ya kuifungia mabao muhimu Simba ikiichapa Coastal Union mabao 2-0 uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Simba ikishangiliwa na mashabiki wake ilijipatia mabao hayo moja kila kipindi na ikijiweka katika mazingira mazuri ya kunyakua kikombe cha ligi kuu bara.
Ushindi wa leo dhidi ya Wagosi wa kaya unawafanya Simba kufikisha pointi 57 huku ikiwa imecheza mechi 24, mshambuliaji Hamisi Kiiza anakuwa amefikisha magoli 19 ni sawa kama ameifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa yupo Yanga Amissi Tambwe aliyewahi kuwa mfungaji bora kwa kufunga magoli 19