MREMBO AMBADILISHA DINI MKOLA MAN, WAZAZI WAKE WAJA JUU

Na Mwandishi Wetu, TANGA

Mwanadada anayefahamika kwa jina la Khadija ambaye ni mwanamitindo inadaiwa anemdatisha kinoma rapa na mtunzi wa nyimbo za 'Multiple Choice', 'Jana na leo' na 'Kitabu' Christopher Mhenga a k a Mkola Man mpaka kufikia kubadilisha dini yake ya ukristo na kuhamia uislamu.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa msanii huyo, amedai Mkola Man haambiwi wala hasikii kwa mwanamke huyo na inadaiwa yuko mbioni kumuoa.

Rafiki huyo ambaye amekataa kutaja jina lake, ameongeza kuwa Mkola Man amebadili dini na sasa ni muislamu anaitwa Mustapha, pia rafiki huyo amedai wazazi wa Mkola Man wamezipata habari hizo za mtoto wao kubadili dini ambapo wamemjia juu.

Wazazi hao wa Mkola Man ni walokole na wameshitushwa na kitendo cha kijana wao kuhamia uislamu lakini wamesema ni uamuzi wake mwenyewe kupenda anapopenda, kuhusu mahusiano kati ya mtoto wao na mrembo huyo, wazazi hao wamemtaka awe mwangalifu kwani wanawake wa sasa wengi wao ni waongo.

"Wanawake wa sasa si wahaminifu kwa wenza wao hivyo kijana wetu awe makini", alisema baba wa msanii huyo ambaye aliwahi pia kujiunga na dini maarufu ya kishetani ya freemason kabla hajaamua kuachana nayo

Mrembo Khadija inadaiwa amemdatisha rapa Mkola Man mpaka kaamua kubadili dini

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA