PLUIJM AIWEKEA MTEGO AL AHLY
Na Salum Fikiri Jr
Kocha mkuu wa Yanga Sc Mholanzi Hans Van der Pluijm anewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa lazima APR ya Rwanda ifungashwe virago katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, lakini watakaokuja mbele yao nao lazima wakalishwe.
Yanga itarudiana na APR jumamosi ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini itakuwa na kazi nyepesi kwani itahitaji matokeo ya sare ya aina yoyote.
Pia itakuwa na faida ya kucheza uwanja wa nyumbani, Yanga itapata sapota ya mashabiki wake hivyo Pluijm anajiamini mno na kudai watawachapa tena, katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Yanga ilishinda 2-1.
Yanga ikivuka hatua hiyo itakutana na mshindi kati ya Al Ahly ya Misri au Recreative Libolo ya Angola, timu hizo zilitoka suluhu 0-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Angola, Yanga inawafahamu vizuri Ahly na iliwakosakosa kuwatoa mwaka juzi kama si Said Bahanuzi kukosa penalti huenda historia ingebadilika.
Pluijm anasema Ahly ni wepesi mno kwao kuliko Libolo kwakuwa hawafahamu, kwahiyo ametamba kuwapangia skwadi ile ile iliyowaua Simba na APR