MABAGA FRESH WARUDI NYUMBANI KIAINA
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
Kundi la muziki wa kufokafoka lililowahi kujipatia umaarufu mkubwa miaka iliyopita la Mabaga Fresh hatimaye wameamua kurudi nyumbani baada ya kimya kirefu.
Akizungumza na mtandao huu, Dj Snox mmoja kati ya wasanii waounda kundi hilo amesema wameamua kurudi nyumbani kwa maana wanaachana na muziki wa Kimarekani na kugeukia muziki wa Kiafrika.
"Tumerudi nyumbani, ndio wimbo wetu mpya tuliouimba kwa mtindo wa Kinanda na Singeli, tumeachana na kopi za Kimarekani kwani mitindo ya Hip Hop na Bongofleva ni za Kimarekani", alisema.
Kundi hilo lililotamba na nyimbo zake kama "Mabaga Fresh tuko kamili", "Mtulize" na nyinginezo ambazo walishirikiana na Juma Nature