UKWELI KUHUSU JKT KANEMBWA NA GEITA GOLD HUU HAPA, TFF WANAPEPESA
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM
Ukweli ni kwamba JKT Kanembwa ya Kigoma tayari ilikuwa ishatelemka daraja, kwahiyo ikaamua kuvunja kambi yake na kuwaruhusu wachezaji wake kurejea makwao, ina maana hata mchezo wao wa mwisho na Geita Gold wasingeingia uwanjani.
Lakini siku ya mchezo wao na Geita Gold chapu chapu viongozi wa Kanembwa waliwapigia simu wachezaji wao ili warejee klabu kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho, walipotua tu na kuingia uwanjani wakapokea mabao 8-0 toka kwa wachimba madini wa Geita Gold Mine wanaonolewa na nahodha wa zamani na kocha wa Simba Seleman Matola.
TFF inachunguza sakata zima la Geita Gold kuishinda Kanembwa 8-0 na Polisi Tabora kuwachapa JKT Oljoro ya Arusha mabao 7-0, madai yaliyopo mezani kwamba timu hizo zimepanga matokeo.
Kama ni kweli timu hizo zilipanga matokeo basi zinaweza kushushwa daraja na kutozwa faini, undani wa sakata hilo TFF wanapepesa macho tu kwani hawajui chochote.
Kuna uwezekano mkubwa timu moja kati ya Polisi Tabora au Geita Gold ikapanda ligi kuu kwavile TFF wanafanya uvunguzi wenyewe bila kuhusisha watu wa Takukuru ambao wanafahamu mazingira ya kuwepo kwa rushwa.
Pia kuna uwezekano mkubwa suala hilo likashindwa kupata ufumbuzi na kusababisha mechi kurudiwa ama laa! Wachezaji wa Geita Gold wakisalimiana na wachezaji wa Simba mjini Geita
. (Picha na Maktaba yetu)