TUNAWACHAPA KWAO CHAD- SAMATTA

Na Elias John, D'jamena

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta amewaahidi ushindi Watanzania dhidi ya Chad mchezo wa kufuzu fainali za mataifa Afrika utakaofanyika Jumatano katika uwanja wa Amnisports Idris Mahamat Ouya.

Nahodha huyo wa Tanzania aliyekabidhiwa mikoba hiyo hivi karibuni akichukua nafasi ya Nadir Ali "Cannavaro" ametamba ni lazima waibuke na ushindi katika mchezo wa leo licha kwamba wanacheza ugenini.

Samatta amedai Tanzania inahitaji kufuzu fainali za mataifa Afrika hivyo hawatakubali iupoteza, aidha pia amedai hiyo haitakuwa kazi nyepesi bali wanahitaji kujituma kwa nguvu zao zote.

Stars inayonolewa na Charles Boniface Mkwassa leo jioni itatelemka dimbani kukwaruzana na wenyeji wao Chad ambao pia watarudiana junatatu ijayo jijini Dar es Salaam.

Hadi sasa Stars ina pointi moja ikiwa imecheza mechi mbili, moja ikichapwa mabao 3-0 na Misri wakati nyingine ikitoka suluhu na Nigeria 0-0, mchezo wa leo utakuwa mkali kwakuwa kila timu inasaka pointi tatu, Kila la kheri Stars

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA