KIKWETE AMLILIA CLUYFF
Na Mwandishi Wetu, TUNISIA
RAIS mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha masikitiko yake na kumlilia gwiji wa zamani wa Barcelona, PSV na timu ya taifa ya Uholanzi Johan Cluyff ambaye amefariki dunia jana kwa naradhi ya saratani.
Kikwete ambaye aliwahi kuzawadiwa jezi na gwiji huyo aliyezaliwa mwaka 1945, Rais mstaafu Kikwete alitoa salamu hizo za pole akiwa mjini Tunis alipokuwa kikazi.
Kikwete ni mwakilishi maalum wa Umoja wa Afrika katika upatanishi wa nchi ya Libya iliyoingia kwenye mgogoro hasa baada ya kuuawa kwa kiongozi wao Muamar Gaddaf ambapo amani haijapatikana hadi sasa.
Katika uongozi wake, Kikwete alikuwa mpenda michezo hasa soka ambapo aliwezesha ziara za klabu kubwa duniani za Real Madrid na Barcelona zote za Hispania ambapo Cluyff naye alibahatika kutua Tanzania na kualikwa Ikulu ya Magogoni na mheshimiwa JK
(Picha chini raisi mstaafu Jakaya Kkwete akikabidhiwa jezi ya Barcelona na Johan Cluyff sasa marehemu, Picha kwa hisani ya Ikulu)