KITABU CHA MKOLA MAN KIKO TAYARI, PRODYUZA WAKE AANIKA KILA KITU
Na Mwandishi Wetu
Hatimaye rapa mwenye maskani yake Hale mkoani Tanga Mkola Man ameachia wimbo wake mwingine unaokwenda kwa jina la "Kitabu cha historia' ambayo imeshasambazwa kwenye mitandao ya kijamii na redio pia.
Akizungumza na mtandao huu, Mkola Man amesema Kitabu kimekamilika na watu kadhaa wameanza kuchangamkia wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wanadownlod kwa wingi.
"Nyimbo yangu nimeirekodi katika studio za K.O Record zilizopo hapa Tanga chini ya prodyuza wangu mahiri Mos ambaye yeye ndiye aliyeibua kipaji changu", alisema.
Aidha Mwandishi wetu alizungumza na prodyuza wa msanii huyo Mos ambapo alimthibitishia kuwa ngoma yake hiyo iko njema na inafanya vizuri, Mkola Man alitamba na wimbo wake wa kwanza wa "Mr Mapesa" alioutengeneza Mos na kwa sasa msanii huyo anaandika "Michano" kupitia blogu hii, Big up Mkola Man