AZAM KIURAHINI LEO KUTINGA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Mrisho Hassan

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azam Fc jioni ya leo wanajitupa uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi kurudiana na Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Azam inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo huo kwani ilijipatia ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini huko Afrika Kusini.

Shukrani kwa mabao ya Shomari Kapombe, Kipre Tchetche na nahodha John Raphael Bocco, hivyo katika mechi yake ya leo itakuwa na kazi nyepesi ambayo itawavusha hadi hatua ya 16 bora.

Lakini vijana wa Bidvest nao wamewasili nchini kwa lengo moja tu ambalo ni kulipiza kisasi, Bidvest siyo timu ya kubeza kwani katika ligi kuu ya Afrika Kusini inashikilia nafasi za juu hivyo lolote linaweza kutokea.

Hadi sasa Tanzania imesaliwa na timu mbili katika michuano ya kimataifa ambazo ni Azam na Yanga ambayo jana ilifanikiwa kutinga raundi ya pili ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA