MICHANO: HAWATOSHEKI NA UKUBWA WA MAJINA YAO, BADO WANAGOMBANIA MAJINA YA WANYAMA

Na Mkola Man, Tanga

Yap...yap...yap..Michano yangu ya leo inawachana chana na kupasua kuhusu kitendo cha wasanii watano wenye majina (Masupa staa) wakubwa ndani na nje ya bongo, wasanii hao kwakweli siwaelewi kabisa maana wanagombania majina ya wanyama wa porini.

Hivi karibuni wasanii watatu waligombania jina la mnyama Simba na kila mmoja akidai ni lake, wasanii hao ni Diamond Platinumz, Mr Blue na Afande Sele "Mfalme", wengine wawili wakigombania jina la Mamba.

Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya na Shetta ama baba Kayla kila mmoja alikuwa akidai yeye ni mamba, wakati mamba wenyewe wanaishi majini na kamwe sijawahi kusikia au kuona mamba akiitwa Dudubaya au Shetta.

Wala sijawahi kuona mnyama simba akiitwa Diamond, Mr Blue au Afande Sele, ila hao wasanii wetu tayari wameshaingia kwenye malumbano ya kugombania haki ya kumiliki jina la mnyama huku majina yao ya kisanii yaliyowapa umaarufu hawatosheki nayo.

Mimi binafsi nimehudhunishwa sana na malumbano hayo, watu wanataka kazi, siyo malumbano, najua wengi wataumia ila lengo langu ni kujenga n si kubomoa, nimeenda mbali sana mpaka kukumbushia ya utotoni.

Tulikuwa tunagombania magari ya kupita barabarani ama ndege ikipita angani mpaka saa nyingine tunagombana mpaka kuzichapa kavu kavu.

Kiufupi wasanii hao waache utoto kugombania kitu ambacho akina uhalisia, watambue simba ni simba na mamba ni mamba, yaap Mkola Man Mwanatanga naondoka zangu na tukutane tena Wiki ijayo ila Happy Birthday Prince Hoza

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA