YANGA YAIWINDA VIKALI NDANDA, KAGERA SUGAR WAJIANDAE
Na Ikram Khamees
Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc wameingia kambini jana kwenye hoteli moja ya kifahari na wakijifua kwenye uwanja wa chuo cha ustawi wa jamii Kurasini tayari kabisa kujiandaa na mchezo wake wa kesho dhidi ya Ndanda Fc.
Yanga kesho jioni itacheza na Ndanda Fc katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa robo fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Yanga itashuka tena uwanja wa Taifa Aprili 3 kukwaruzana na Kagera Sugar mchezo wa ligi kuu bara, pia itatelemka tena uwanja huo huo wa Taifa Aprili 6 kuvaana na Mtibwa Sugar.
Yanga imeamua kuingia kambini kujiandaa na mechi hizo kwani Aprili 9 itacheza na Al Ahly ya Misri mchezo wa raundi ya pili ligi ya mabingwa barani Afrika