YANGA YATINGA RAUNDI YA PILI AFRIKA

Na Prince Hoza

Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc jioni ya leo wamefanikiwa kuvuka hadi raundi ya pili ya ligi ya mabingwa barani Afrika licha ya kulazimishwa sare ya wageni APR ya Rwanda ya kufungana 1-1 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga ilianza ikiwa kama imezidiwa kwani dakika ya tatu kipindi cha kwanza iliruhusu bao lililofungwa na Erick Lusanga ambaye leo aliihenyesha mno Yanga.

Hata hivyo Yanga waliweza kujirekebisha na kucheza kandanda la kuelewana na katika dakika ya 25 kipindi hicho hicho cha kwanza walifanikiwa iusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Donald Ngoma aliyewatoka mabeki wa APR.

Hadi mapumziko matokeo no hayo hayo, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kumshambulia mwenzie lakini hakukuwa na goli, Yanga sasa imefuvu raundi ya pili kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya ushindi wa 2-1 ilioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Kigali Rwanda.

Ina maana Yanga itakutana na Al  Ahly ya Misri kwani katika mchezo wake wa leo dhidi ya Reacreative Libolo ya Angola walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0