AZAM YAZIFUATA SIMBA NA YANGA ROBO FAINALI FA CUP
Na Mrisho Hassan, Moshi Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Azam Federation Cup ama kombe la FA baada ya kuilaza FC Panone ya Kilimanjaro mabao 2-1 uwanja wa Ushirika Moshi. Vijana wa Panone wanaonolewa na kocha wa zamani wa Yanga na JLT Ruvu walikuwa wa kwanza kujipatia bao la kuongoza lililofungwa na Geofrey Mbuda aliyetumia vema makosa ya beki wa Azam Paschal Wawa. Azam nao walisawazisha bao hilo kupitia kwa beki wake Paschal Wawa aliyerekebisha makosa yake, Azam walingeza bao la pili na la ushindi lililofungwa na mshambuliaji Alan Wanga. Kwa matokeo hayo Azam imeingia robo fainali ya michuano hiyo hivyo inaingana na Simba, Yanga, Mwadui, Coastal Union, Geita Gold, Ndanda na Prisons