AZAM YAZIFUATA SIMBA NA YANGA ROBO FAINALI FA CUP

Na Mrisho Hassan, Moshi

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Azam Federation Cup ama kombe la FA baada ya kuilaza FC Panone ya Kilimanjaro mabao 2-1 uwanja wa Ushirika Moshi.

Vijana wa Panone wanaonolewa na kocha wa zamani wa Yanga na JLT Ruvu walikuwa wa kwanza kujipatia bao la kuongoza lililofungwa na Geofrey Mbuda aliyetumia vema makosa ya beki wa Azam Paschal Wawa.

Azam nao walisawazisha bao hilo kupitia kwa beki wake Paschal Wawa aliyerekebisha makosa yake, Azam walingeza bao la pili na la ushindi lililofungwa na mshambuliaji Alan Wanga.

Kwa matokeo hayo Azam imeingia robo fainali ya michuano hiyo hivyo inaingana na Simba, Yanga, Mwadui, Coastal Union, Geita Gold, Ndanda na Prisons

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI