PRISONS YAISHIKISHA ADABU MBEYA CITY

Na Alex Jonas, Mbeya

Tanzania Prisons jioni ya leo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya imewaadhibu mahasimu wao Mbeya City mabao 2-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la FA.

Mabao ya Mohamed Mkopi na kipa Benno Kakolanya yalitosha kabisa kuwapa uahindi maafande hao, goli la kwanza la Prisons lilifungwa kipindi cha kwanza na la pilj lilifungwa kipindi cha pili.

Licha ya Mbeya City kujitutumua angalau kusawazisha lakini ilishindikana kwani vijana wa Prisons walikuwa imara, goli la kufutia machozi la Mbeya City lilifungwa na Joseph Mahundi.

Hata hivyo goli lililofungwa na kipa wa Prisons Benno Kakolanya limeingia katika rekodi ya aina yake, Kakolanya anakuwa kipa wa tatu kufunga.

Iddi Pazzi 'Father' na Juma Kaseja ndio makipa pekee waliofanikiwa kufunga, Pazzi alifunga mwaka 1984 alipokuwa anaidakia Simba na Kaseja alifunga mwaka 2013 alipokuwa Yanga Sc

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA