NI SIMBA AU YANGA NANI ATACHEKA BAADA YA DAKIKA 90

Na Alex Jonas

Ni pambano la kihistoria linatarajia kupigwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam ambapo miamba ya soka nchini Simba na Yanga itakapepetuana.

Timu zote zimejiandaa kuelekea mchezo huo ambapo kila moja iliweka kambi nje ya jiji kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.

Simba ambao ni vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 45 waliweka kambi yao mjini Morogoro, Simba ina kumbukumbu nzuri ya kushinda mechi sita mfululizo.

Kikosi cha Simba kinachonolewa  na Jackson Mayanja kina hali nzuri ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo, Simba inajivunia washambuliaji wake wanne Hamisi Kiiza, Ibrahim Ajibu, Danny Lyanga na Mwinyi Kazimoti.

Bila shaka nashabiki wake wanajipa matumaini ya kuondoka na ushindi mbele ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu bara.

Yanga wao waliweka kambi yao Pemba ambapo wana kumbukumbu napo kwani katika mchezo wao wa kwanza na Simba walikaa eneo hilo na wakashinda mabao 2-0.

Hivyo mashabiki wake wanaaminj leo watatoka na ushindi, Yanga inayonolewa na Mholanzi Hans Pluijm itawategemea zaidi Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Thabani Kamusoko.

Bila shaka mchezo huo utakuwa mkali na wa kuvutia, wakati miamba hiyo ikiumana Taifa, jijini Mbeya matajiri wa bongo Azam Fc wana kibarua kigumu watakapocheza na wagonga nyundo wa Mbeya City

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA