YANGA YAIENDEA AZAM FC PEMBA

Na Ikram Khamees, Pemba

Vinara wa ligi kuu bara Yanga Sc inatarajia kuwasili visiwani Pemba tayari kabisa kujiandaa na mchezo wake wa ligi jumamosi ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya waoka mikate wa Azam Fc.

Yanga imeamua kuijia Azam Pemba ni kutokana na ushndani wake unapokuwa mkubwa hivyo imeamua kuijia Pemba kama ilivyofanya hivyo dhidi ya Simba Sc.

Yanga iliijia Simba Pemba na ikafanikiwa kuichapa mabao 2-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa ligi kuu bara.

Vinara hao wa ligi kuu ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo na safari hii inataka kuhakikisha inachukua tena ubingwa, Akizungumza jana na blogu hii msemaji wavYanga Jerry Muro amesema Yanga itaweka kambi yake Pemba ili kujiandaa na Azam.

Muro amedai Pemba ni sehemu tulivu hivyo panafaa kwa kambi, ameongeza Azam inawakamia sana hasa wanapokutana nao lakini safari ya Pemba itakuwa mwisho wao.

Amedai kikosi chao lazima kiibuke na ushindi katika mchezo huo ili iendelee kuongoza ligi kwa uwiano wa pointi, kwa sasa Yanga inaongoza ligi kwa uwiano wa magoli kwani yenyewe ina pointi 46 sawa na Azam

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA