MWANAMAMA KUAMUA MTANANGE WA WATANI JUMAMOSI, VIINGILIO VYATAJWA
Na Mrisho Hassan
Mwamuzi wa kike Jonnesia Rukyaa ndiye atakayepuliza kipyenga jumamosi katika mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mwamuzi huyo ndiye aliyechezesha wakati miamba hiyo ilipokutana nwaka juzi mchezo wa Nani Mtani Jembe Simba ikishinda 2-0 magoli yakifungwa na Awadh Juma na Elius Maguli.
Wakati Baraka Kizuguto akiwatangazia waandishi wa habari leo, pia alitaja viingilio katika mchezo huo ambapo kwa upande wa walalahoi itakuwa shilingi 7000 na kule wanapokaa matajiri yaani V.I.P shilingi 30, 000.
Simba na Yanga zinatarajia kupambana siku ya jumamosi mchezo wa ligi kuu bara, katika mchezo wa raundi ya kwanza Yanga iliifunga Simba mabao 2-0