MALINZI ATAKIWA KUJIUZURU

Na Prince Hoza

Wadau wa michezo nchini wamemtaka rais wa shirikisho la kandanda nchini TFF Jamal Malinzi ajiuzuru nafasi hiyo kutokana na kashfa ya upangaji matokeo ligi Daraja la kwanza Tanzania bara (FDL).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wamesema, Malinzi amekuwa mstari wa mbele kutetea maovu yanayofanywa na watendaji wake ikiwemo suala la kuiruhusu Azam Fc kwenda Zambia kushiriki bonanza.

Rais huyo wa TFF aliomba radhi kwa kitendo hicho kwani wakati Azam inaondoka nchini, ilitakiwa kucheza mechi zake mbili za ligi, Malinzi anatakiwa kujiuzuru ili kulinda heshima yake.

Bosi huyo wa TFF anatajwa kuhusika na upangaji wa matokeo uliozikuta timu za Geita Gold Fc na Polisi Tabora, timu hizo kila moja ilipata ushindi wa kushangaza.

Geita Gold Fc iliifunga JKT Kanembwa ya Kigoma mabao 8-0, wakati Polisi Tabora nayo ikaichapa JKT Oljoro mabao 7-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA