WACHEZAJI YANGA WAWANYOOSHEA SIMBA VIDOLE VITANO

Na Alex Jonas, Pemba

Tayari mabingwa wa soka nchini Yanga Sc wamewasili Pemba kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaochezwa jumamosi ijayo na mtani wake Simba Sc katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga jana ilikuwa katika ardhi ya Mauritius ambapo saa 9:30 ilipepetana na Cercle de Joachim katika uwanja wa Curepipe mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika.
Katika mchezo huo Yanga imechomoza na ushindi wa bao 1-0 ambapo itakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano jijini Dar es salaam majuma mawili yajayo.
Donald Ngoma ndiye mfungaji pekee wa goli la ushindi la Yanga, lakini hesabu zote za Yanga zimeelekezwa kwenye mchezo wa jumamosi dhidi ya Simba na iliamua kukodi ndege ya kuwapeleka Mauritius kisha kuwapeleka Pemba kabla ya kuwaleta Dar es salaam.
Walipotua kisiwani Pemba muda huu, wachezaji wa Yanga waliwaonyeshea vidole vitano mashabiki wa Simba, hiyo ina maana kwamba Yanga itawafunga Simba mabao matano.
Ama ishara hiyo inawakumbusha deni walilonalo kwa Simba hasa mwaka 2011 Yanga ikichapwa mabao 5-0 na Simba katika uwanja huo huo wa Taifa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA