DONALD NGOMA AIPAISHA YANGA KIMATAIFA, YASHINDA 1-0
Na Alex Jonas, Curepipe
Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imeanza vema michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuilaza 1-0 timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika uwanja wa Curepipe.
Mabingwa hao ambao leo wamepokwa uongozi wa ligi kuu bara na mtani wake Simba watakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano utakaofanyika jijini Dar es salaam wiki mbili zijazo.
Mshambuliaji Donald Ngoma raia wa Zimbabwe aliifungia Yanga bao la ushindi na kuifanya itoke kifua mbele.
Yanga sasa inarejea na ndege yake ya kukodi na moja kwa moja itaelekea Pemba kuweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa ligi kuu bara dhidi ya hasimu wake mkubwa Simba katika uwanja wa Taifa Dar es salaam