PRISONS YAISHIKA MBAYA AZAM FC
Na Saida Salum Mbeya
Wajelajela Prisons jioni ya leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeilazimisha sare ya 0-0 Azam Fc mchezo wa ligi kuu bara.
Azam Fc ikiwa na washambuliaji wake mahiri John Raphael Bocco, Kipre Herman Tchetche na kiungo wake Abubakar Salum lakini walishindwa kupenya ukuta wa vijana hao walioongozwa na beki Nurdin Chona.
Prisons ambao wako katika kiwango cha juu msimu huu mara kwa mara walijaribu kulifikia lango la Azam kutaka kufunga lakini ngome ya waoka mikate hao iliyokuwa ikiongozwa na Paskal Wawa.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi 46 na imeshindwa kuitoa Yanga kileleni hivyo itasalia katika nafasi yake ileile ya pili