KAMUSOKO AWATUMBUA JIPU JKT MLALE, SASA WATINGA ROBO FAINALI
Na Mrisho Hassan
Mabingwa wa soka nchini na vinara wa ligi kuu bara Yanga Sc jioni ya leo imewatumbua jipu wanajeshi wa JKT Mlale ya Ruvuma baada ya kuwachapa mabao 2-1 uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa kombe la FA.
Yanga moja kwa moja imesonga hadi robo fainali ya michuano hiyo na imekuwa timu ya kwanza kufanya hivyo.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo hasa baada ya wikiendi iliyopita kuichapa Simba Sc mabao 2-0 mchezo wa ligi kuu bara katika uwanja huo huo wa Taifa.
Yanga ambayo jumamosi ijayo itashuka uwanja wa Taifa kuvaana na Cercle de Joachim ya Mauritius mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Afrika, iliutumia mchezo wa leo kama maandalizi.
Vijana wa JKT Mlale walikuwa wa kwanza kupata bao lakini Geofrey Mwashiuya kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Simba ambapo alipiga krosi murua ikiyotua kwenye mguu wa Amissi Tambwe, leo alifanya hivyo na kumkuta Paul Nonga na kuisawazisbia Yanga.
Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe alitumia vema krosi ya Mwashiuya na kuipatia Yanga bao la ushindi na kutinga robo fainali