AZAM FC NA PRISONS, NGOMA INOGILE

Na Saida Salum, Mbeya

Kesho ndiyo kesho katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya wakati wenyeji Tanzania Prisons watakapoikaribisha Azam Fc mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Azam Fc wataingia uwanjani kwa lengo la kutwaa pointi zote tatu ili ikamate usukani wa ligi kuu bara, kikosi cha Azam kina kumbukumbu nzuri kwani jumamosi iliyopita iliifunga Mbeya City mabao 3-0 katika uwanja huo huo wa Sokoine.

Akizungumza na blogu hii jana, msemaji wa Azam Jaffari Idd amesema timu yake lazima ipate ushindi kwakuwa vijana wake wako vizuri.

Azam itamkosa kiungo wake mahiri Himid Mao mwenye kadi tatu za manjano, nao vijana wa Prisons wamejinasibu kuondoka na ushindi katika mchezo huo.

Vijana hao wa jeshi la Magereza, wamesema Azam ni timu ya kawaida kama nyingine walizowahi kukutana nazo hivyo wategemee kipigo kutoka kwao, Prisons wana kumbukumbu ya kuizuia Yanga baada ya kuilazimisha sare ya mabao 2-2 katika uwanja huo huo wa Sokoine

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA