NILITABIRI YANGA ITASHINDA 3-0 LAKINI NIYONZIMA KANITIBUA- MUUMINI MWINJUMA
Na Saida Salum
Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi ya Double M, Muumin Mwinjuma akiwa na familia yake baada ya furaha kubwa aliyonayo kufiatia timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya hasimu wake mkuu Simba uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.
Awali Muumin alijua wazi kama Yanga itaibuka na ushindi wa mabao 3-0 lakini haikuwa hivyo na jana ikishinda 2-0 na kujiongezea pointi tatu muhimu.
"Nilitabiri Yanga itashinda 3-0 lakini Haruna Niyonzima ameniudhi jana baada ya kukosa goli la wazi, Simba sasa hivi ni wateja wetu hawatiwezi tena na tutawanyanyasa sana", alisikika Muumin ambaye alikuwa Pemba ya Msumbiji na bendi yake.
Mashabiki wa Yanga jana walikuwa na furaha hasa baada ya timu yao kuichapa Simba mabao 2-0 mchezo wa ligi kuu bara, magoli ya Yanga yalitiwa kimiani na Donald Ndombo Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Joselyin Tambwe raia wa Burundi