SIMBA WASHITUKIA KAMBI YA ZANZIBAR, SASA WAAMUA KUBAKI MOROGORO, WADAI YANGA AKITOKA JUMAMOSI WAKATAMBIKE

Na Prince Hoza, Morogoro

Vinara wa ligi kuu bara Simba Sc wameamua kujichimbia mjini hapa na kuachana na kambi ya Zanzibar wakidai imezingirwa na ushirikina mwingi.
Mmoja kati ya viongozi wa timu hiyo aliyeambatana na timu tangia mjini Shinyanga ameamua kufichua kilichopelekea timu yao kujificha Moro na kuikacha Zanzibar.
Kiongozi huyo aliyekataa kutaja jina lake akidai yeye si msemaji wa klabu amethibitisha kuwa ile kambi yao ya Zanzibar tayari imezingukwa na watu wa Yanga hivyo hawataweza kwenda
"Simba kwa sasa itaendelea kujificha Moro na vijana wako katika hali nzuri na jumamosi Yanga lazima afe" alisema kiongozi huyo anayekubalika na wanachama wa klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Simba na Yanga zinakutana jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mchezo wa ligi kuu bara.
Yanga wameweka kambi yao Pemba, katika mchezo wa kwanza Yanga iliweka kambi yake Pemba na Simba walijificha Unguja, lakini zilipokutana uwanja wa Taifa, Yanga ilishinda mabao 2-0.
Lakini safari hii Simba wameshituka kidogo na hawataki kwenda kujificha Unguja kwani eneo wanalokaaga Yanga wameshafanya yao hivyo sasa wanakomaa Morogoro na mwenyekiti wake wa kamati ya usajili Zacharia Hanspoppe ametamba Simba itashinda mchezo huo.
Hanspoppe amedai vijana wake wako imara na sasa wanaingoja Yanga tu, aidha kigogo huyo amedai kama Yanga itasalimika basi wakatambike

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA