YANGA YATINGA RAUNDI YA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Na Prince Hoza

Wawakilishi wa Tanzania Yanga Sc jioni ya leo imefuzu raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuilaza Cercle de Joachim ya Mauritius mabao 2-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Licha ya mchezo huo kutokuwa wa ushindani mkubwa, lakini vijana wa Yanga walicheza kandanda safi na la kuvutia.

Mabao yaliyopatikana dakika ya tatu kipindi cha kwanza na dakika 12 kipindi cha pili yaliyofungwa na Amissi Joselyin Tambwe raia wa Burundi na Thabani Scara Kamusoko raia wa Zimbabwe yalitosha kabisa kuwapeleka Yanga raundi ya kwanza.

Kwa maana hiyo Yanga itakutana na APR ya Rwanda au Mbabane Swallors ya Swaziland, ushindi ilioupata leo unaifanya Yanga iwaondoe mashindanoni Cercle de Joachim kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0.

Yanga sasa itarejea kwenye ligi kuu bara jumatano itakaoikaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Taifa Dar es Salaam na jumamosi ijayo itavaana na Azam Fc

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA