TFF YAPINGA MATOKEO YA GEITA, POLISI TABORA, SASA KAMATI YA NIDHAMU KUAMUA
Na Mrisho Hassan
Kamati iliyokutana masaa 72 jana ya shirikisho la kandanda nchini TFF ineyapinga matokeo ya kundi C ligi Daraja la kwanza Tanzania kati ya Geita Gold na JKT Kanembwa iliyochezwa uwanja wa Lake Tanganyika na ule kati ya Polisi Tabora na JKT Oljoro uliofanyik uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.
Kamati hiyo ya masaa 72 imepinga vikali ushindi wa Geita Gold wa mabao 8-0 dhidi ya JKT Kanembwa na ule wa Polisi Tabora kuifunga JKT Oljoro mabao 7-0.
Madai ya kamati hiyo kupinga ushindi huo imegundua kuwepo kwa mazingira ya upangwaji matokeo, hivyo kamati hiyo imeshindwa kutangaza timu iliyopanda ligi kuu na sasa imepeleka suala hilo kwenye kamati ya nidhamu ya TFF.
Ikithibitika timu hizo zilipanga matokeo zitashushwa daraja na kutozwa faini kubwa ili iwe fundisho kwa wengine