MICHANO: RITTA PAULSEN WA (BSS) NAYE NI JIPU
Na Mkola Man, Mwanatanga
Yap yap yap leo michano yangu inaichana Bongo Star Search (BSS) hasa mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo la BSS, Ritta Paulsen au Madame Ritta.
Mimi hapa (Mkola Man) namfananisha Madame Ritta na mkulima ambaye anapanda michungwa isiyozaa machungwa, kutokana na kutoipalilia toka mwaka 2007 Jumanne Idd, 2008 Misoji Nkwabi, 2009 Paschal Cassian, 2010 Mariam Mohamed,, 2011 Hajji Ramadhan, 2012 Waltel Chilambo, 2013 Emmanuel Msuya na mwaka 2014 hayakufanyika.
Shindano hilo likarudi tena mwaka jana 2015 na akashinda Kayumba Juma, mchungwa huu unaanza kutoa maua hasa baada ya kufyekewa na kukutwa na mvua.
Hii yote imetokana na uwepo wa Mkubwa Fella na Babu Tale, je mashindano ya huko nyuma yalikuwa na dhamila ya kweli ya kuinua vipaji au dhamila ya upigaji?.
Ritta Paulsen kwa BSS yako umeshatuweka njia panda, hujawasaidia kidhati washindi, zipo BSS nyingi duniani ikiwemo ile ya American Star Search ambayo ilimtoa kimuziki mshindi wake Ruben Studdad, wewe Ritta ulitaka fedha tu na umaarufu na siyo kuendeleza vipaji.
Tukutane tena wiki ijayo, Kwa maoni, au kama unataka jambo flani niliandike au kitu au mtu tumchane nicheki kwa namba yangu ya mkononi 0715281223, MwanaTanga