AZAM FC YASHINDWA KUKWEA KILELENI, YAPIGWA 1-0 NA COASTAL UNION

Na Saida Salum, Tanga

Mabingwa wa soka Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo imepokea kichapo toka kwa wenyeji wao Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Azam ambayo sasa inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42 imeshindwa kukwea kileleni hivyo inawafanya Wekundu wa Msimbazi kuendelea kukaa kileleni na pointi zao 45 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 43.
Coastal Union ambao wamekuwa wakifanya vibaya wanapocheza na timu dhaifu lakini imekuwa ikitoa vipigo kwa vigogo ambapo ilianza kuitandika Yanga Sc.
Goli la ushindi la Coastal Union limefungwa na muuaji wake yule yule aliyeiua Yanga Miraji Adamu, hata hivyo nahodha wa Azam alitaka kurushiana makonde na wenzake wa Coastal.
Kwa maana hiyo Azam itakuwa na kazi ngumu ili iweze kurejea tena kileleni kwani jumamosi ijayo itacheza na Mbeya City iliyorejea katika makali yake baada ya kupata kocha mpya raia wa Malawi Kinah Phiri

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA