SIMBA YAKUBALI KUWA TEJA LA YANGA, RASMI YAREJEA KILELENI, BOSSOU AMPOTEZA VIBAYA KIIZA
Na Alex Jonas, Uwanja wa Taifa
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imeendeleza undava kwa watani zake Simba Sc baada ya kuichapa mabao 2-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe yametosha kabisa kuipa pointi tatu na magoli mawili Yanga na kuifanya irejee kileleni ikiwa na pointi zake 46.
Simba iliutawala mchezo kipindi cha kwanza na kuwafanya mashabiki wake kuamini leo wataibuka na ushindi, Yanga haikucheza vizuri kipindi cha kwanza lakini ilitumia vema nafasi iliyoipata.
Mlinzi wa Yanga Vincent Bossou raia wa Togo ambaye hivi karibuni alizungumza na blogu hii kuwa hamuogopi kabisa Hamisi Kiiza "Diego" kwani ana uwezo mkubwa wa kuwadhibiti washambuliaji machachari.
Bossou leo amemkaba vilivyo Kiiza na kumpoteza kabisa mpaka kocha wa Simba Jackson Mayanja kumtoa, Ibrahim Ajibu naye alidhibitiwa vikali mpaka kutolewa, beki Abdul Banda alionyeshwa kadi nyekundu na kuifanya icheze ikiwa pungufu