BOSSOU- BADO TCHETCHE

Na Alex Jonas

Mlinzi wa kati wa Yanga Vincent Bossou raia wa Togo ambaye jumamosi iliyopita alimdhibiti vilivyo mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati miamba Simba na Yanga ilipokutana.

Beki huyo wa kati aliyecheza kistadi na kumzuia kabisa kinara huyo wa mabao ligi kuu bara wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Tambwe wa Burundi.

Bossou ambaye aliwahi kufanya mazungumzo na blogu hii kule Pemba ambapo alidai ni kazi ndogo sana kumdhibiti mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza kwani aliweza kumkaba Didier Drogba wa Ivory Coast.

Hata hivyo Bossou aliweza kumkaba Kiiza mpaka alipotolewa na kumpisha mchezaji mwingine baada ya kuchemsha, sikia anachosema Bossou.

Beki huyo mrefu mwenye nguvu ametamka maneno mengine ambayo kama yatasikilizwa na Kipre Tchetche basi anaweza akachukia, Bossou amedai anamtamani sana Tchetche na amesisitiza watakapokutana hivi punde atamjua yeye ni nani

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA