YANGA LEO NI MWENDO WA KUJIPIGIA TU
Na Saida Salum
Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc jioni ya leo inajitupa uwanja wa Taifa Dar es salaam kukabiliana vikali na Cercle de Joachim ya Mauritius mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika.
Yanga inaingia uwanjani ikiwa na faida ya goli moja ililolipata mjini Curepipe ilipocheza mchezo wa kwanza.
Donald Ngoma mfungaji wa goli hilo pekee atakosekana katika mchezo huo baada ya majuzi kusafiri kuelekea Zimbabwe ambapo mdogo wake alifariki uwanjani.
Ngoma mchezaji tegemeo wa Yanga kwani ndiye aliyeipa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mtani wao Simba Sc uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga itajivunia mgambuliaji wake Amissi Tambwe na Malimi Busungu wakisaidiwa na viungo Simon Msuva, Geofrey Mwashiuya na Deus Kaseke.
Lakini pia inapaswa kuwachunga sana Cercle de Joachim kwani si timu ya kubeza, endapo Yanga itasonga mbele itaingia raundi ya kwanza na huenda ikakutana na APR ya Rwanda au Mbabane Swallons ya Swaziland