STAA WETU: JERRY TEGETE WA MWADUI FC YA SHINYANGA
Na Salum Fikiri Jr
Ni mchezaji wa Mwadui Fc anayecheza nafasi ya ushambuliaji, mpaka sasa ameshafunga jumla ya mabao matano, na ana kiu ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Jerry Tegete alikuwa mitaa ya Jangwani akiichezea Yanga Sc kwa mafanikio makubwa hasa akichangia kuipa mataji manne, mawili ya kombe la Kagame.
Mshambuliaji huyo mrefu aliibuliwa na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Mbrazil Marcio Maxinmo.
Mara ya kwanza Maximo alilaumiwa na wadau wa soka nchini hasa pale alipoonekana akimkumbatia Tegete, lakini baadaye nyota yake ilianza kung' ara na ndipo Simba na Yanga zilipopigana vikumbo kumwania.
Jerryson Johnson Tegete alijiunga na Yanga na alidhihirisha makali yake na wala Maximo hakukosea kumchukua kutoka shule ya sekondari ya Makongo High School.
Tegete alifanikiwa kuitungua Simba zaidi ya mara mbili na kumfanya azidi kuogoewa, mshambuliaji huyo mbali na kutegemewa na Yanga, pia alikuwa tegemeo kwenye timu ya taifa.
Tegete ni mtoto wa kocha wa Toto African ya Mwanza John Tegete, msimu huu amejiunga na Mwadui Fc ya Shinyanga inayoshiriki ligi kuu bara.
Mwadui inayonolewa na kocha mbwatukaji Jamhuri Kihwelu "Julio" imekuwa ikimtegemea sana mshambuliaji huyo ambaye ameahidi kula sahani moja na Amissi Tambwe na Hamisi Kiiza ambao kila mmoja ana mabao 14 na wako kileleni kwa mabao