RACHEL BITHULO NDANI YA TUZO ZA NYAMBAGO
Na Prince Hoza
Mwigizaji chipukizi wa filamu nchini Bongo Muvi, Rachel Bithulo "Recho" kesho atakuwa ndani ya tuzo za Nyambago zinazotarajia kufanyika mjini Dodoma.
Akizungumza na blogu hii, Recho amesema amefanikiwa kuingia kwenye tuzo hizo kama mwigizaji bora wa kanda ya kati.
Amewataka wapenzi wake na mashabiki kuendelea kumpigia kura ili aibuke kidedea, msanii huyo ambaye pia ni Video Queen wa muziki wa bongofleva, alifanya vizuri kwenye wimbo wa "Yuleyule' wa msanii PNC.
Recho ameigiza vizuri katika filamu ya Craritta ambayo imemfanya aingie kwenye tuzo hizo, "Malengo yangu ni kuchukua tuzo, naomba sapoti zenu wadau kwani ushindi wangu ni wetu sote" alisema msanii huyo mwenye asili ya Usukumani