YONDANI AWAUMIZA VICHWA YANGA
Na Alex Jonas
Kufuatia shirikisho la kandanda nchini TFF kumfungia mechi tatu beki wa Yanga Kevin Yondan tayari kumeanza kuwaumiza vichwa baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Yanga.
Yondani alifungiwa mechi tatu na TFF baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga na Coastal Union uliofanyika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Beki kisiki wa Yanga alimrushia box la dawa daktari wa Coastal Union anayefahamika kwa jina la Mganga, kitendo hicho kilipelekea kuonyeshwa kadi nyekundu.
Yondan amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya shilingi laki tano, hata hivyo tayari ameshatumikia mechi mbili dhidi ya Prisons ya Mbeya na JKT Ruvu.
Mchezaji huyo ataukosa mchezo dhidi ya Simba hivyo Wanayanga wameanza kuingiwa kiwewe wakiamini fowadi ya Simba inayoongozwa na Hamisi Kiiza na Ibrahim Hajibu itawasumbua mara kwa mara.
Yanga kwa sasa imekuwa ikiwatumia Vincent Boosou na Mbuyu Twite na umekuwa ukiruhusu magoli ya kizembe, Nadir Haroub "Cannavaro" ambaye ni majeruhi huenda akachezeshwa ili mradi kumdhibiti Kiiza