AZAM FC YAENDELEA KUITAMBIA MBEYA CITY

Na Salum Fikiri Jr, Mbeya

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuilaza Mbeya City mabao 3-0 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya mchezo wa ligi kuu bara.

Ushindi huo unaipeleka Azam hadi nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga, Azam imefikisha pointi 45 sawa na Simba lakini ina wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Mabao ya Azam ambayo jumla imeibuka mbabe kwa Mbeya City mara nne, yalifungwa na washambuliaji wake Kipre Tchetche, John Raphael Bocco na kinda Farid Mussa.

Kocha wa Azam Muingereza Stewart Hall amesema timu yake ilistahili matokeo hayo kutokana na maandalizi mazuri ya vijana wake baada ya kufuta makosa katika mchezo wao dhidi ya Coastal Union ambapo Azam ililala 1-0 Mkwakwani Tanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI