A,ZAM FC YAZIFUATA SIMBA, YANGA ROBO FAINALI YA FA
Na Mrisho Hassan, Moshi
Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la FA baada ya kuichapa Panone Fc ya Kilimanjaro katika uwanja wa Ushirika Moshi.
Wenyeji Panone wanaonolewa na Fred Felix Mjnziro ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Geofrey Mbuda.
Goli hilo lilitokana na makosa ya mabeki wa Azam ambao walishindwa kuuokoa mpira ulioelekezwa langoni mwao.
Beki Paschal Wawa ambaye alihusika katika makosa ya kuruhusu bao, alisawazisha makosa yake na kuipatia Azam bao la kusawazisha kabla ya mshambuliaji Mkenya Alan Wakende Wanga kuongeza bao la pili.
Kwa matokeo hayo Azam imetinga robo fainali ya michuano hiyo inayofahamika kama Azam Federation Cup, kwa maana hiyo Azam inaungana na miamba ya soka nchini Simba na Yanga kucheza hatua hiyo.
Timu nyingine zilizofuzu ni Coastal Union ya Tanga, Ndanda ya Mtwata, Mwadui ya Shinyanga, Geita Gold ya Geita na Prisons ya Mbeya