NEY WA MITEGO AMPA SHAVU LA NGUVU RAY

Na Shafii Hoza

Msanii maarufu wa filamu Bongo Movie Vincent Kigosi "Ray" anatarajia kuanzisha kampeni itakayomwezesha kupiga mkwanja wa nguvu.

Akizungumza hivi karibuni, Ray amesema anatarajia kuanzisha kampeni ya nguvu ya kuwahamasisha watu kunywa maji kwa wingi ili kuimarisha afya zao ikiwemo kuimarisha ngozi zao.

Ray ametajwa kwenye wimbo wa msanii Ney wa Mitego kuwa anatumia fedha nyingi kwa ajili ya kujiremba na kununua mkorogo ili awe mweupe.

Pia msanii huyo ambaye wimbo wake uitwao "Shika adabu yako" unefungiwa na BASATA, Ray ametajwa tena kwenye wimbo huo ikiwa bado anaishi kwa wazazi licha kwamba ni mkubwa.

Hata hivyo baada ya kuhit kwa wimbo huo, msanii Ray aliibuka na kukanusha vikali kuwa yeye hatumii mkorogo isiokuwa anakunywa sana maji na kufanya mazoezi.

Pia akadai anaendelea kuishi kwa wazazi kwa sababu mama yake hataki ahame, tangia Ray alipotoa majibu hayo, tayari watu wengi wameokana kufurahia majibu yake na wengi wakionekana wanakunywa maji kwa wingi ili na wao wawe weupe.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA