SIMBA YAINYANYASA SINGIDA UNITED
Na Ikram Khamees
Simba Sc jioni ya leo imevuka hatua ya robo fainali michuano ya kombe la TFF baada ya kuilaza Singida United mabao 5-1 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi walipata mabao kupitia kwa Awadh Juma "Maniche" na Hamisi Kiiza "Diego" ambao wote wamefunga mawili kila mmoja na lingine limefungwa na Danny Lyanga.
Kwa matokeo hayo Simba imetinga robo fainali ikiungana na mtani wake Yanga Sc ambayo jumamosi iliyopita iliwalaza mabao 2-0.
GeitavGold Fc nayo imetinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuilaza Toto Africans ya Mwanza bao 1-0 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Baada ya ushindi wa mechi ya leo, Simba inajiandaa na mchezo wake wa ligi kuu bara dhidi ya Mbeya City jumamosi