"KIKWETE ALINIPA MILIONI 18 YA KUNUNULIA KIWANJA"- MPOTO
Na Prince Hoza
Msanii wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto "Mpoto" amefichua uswahiba wake na aliyekuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete kuwa aliwahi kuzawadiwa shilingi milioni 18 ili anunue kiwanja.
Akizu gumza hivi karibuni, Mpoto amesema, Kikwete alikuwa mpenzi mkubwa wa kazi zake hasa baada ya kurekodi wimbo wake wa "Mjomba" ambao baadaye ulimkutanisha na rais Kikwete, akisema.
"Kikwete kupitia msaidizi wake Januari Makamba wakiniita na kudai wimbo wa Mjomba ulimlenga moja kwa mjomba JK, hata hivyo Makamba alisifu mashairi yangu na kuniambia kitu kuwa mheshimiwa rais wakati huo alifurahishwa nao", aliongeza.
"Nilipokutana naye nchini Ufaransa, Kikwete aliahidi kunipatia shilingi milioni 18 huku akidai ni shabiki wa muziki wangu, niluporudi Tanzania, nilienda Ikulu ambapo walinipa fedha hizo", alifichua mwanamuziki huyo anayemsifu Kikwete kwa kusaidia maendeleo ya sanaa nchini