MICHANO: NEY WA MITEGO ANAJIPUNGUZIA MASHABIKI AU!
Na Mkola Man Mwanatanga
Yap yap yap leo nachana kuhusu nyimbo ya Ney wa Mitego iitwayo "Shika adabu yako" ambayo ndiyo habari ya mjini na vijijini.
Kutokana na utandawazi, Ney wa Mitego amejiongezea mashabiki, pia amejipunguzia mashabiki, vijana wengi wa kiume tumeweza kumpongeza kwa ujasili wake, ila imekuwa tofauti na dada zetu.
Dada ,zetu wao asili yao huruma na kupenda mambo mazuri tuu, kiukweli amewagawa mashabiki wake huku akijua ana mtaji mdogo wa mashabiki.
Pia wale anaowachana kwenye nyimbo zake wana mitaji mikubwa ya mashabiki, kwa mfano Ray na Ommy Dimpoz, sijajua ana mbinu gani kutokana na mitego yake.
Ney wa Mitego anawagawa mashabiki wake yeye mwenyewe nyimbo zake za kuwachana wenzake, Mkola Man "Mwanatanga" sina makuu ila namchukulia kijana huyu mwenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro sawa na mfugaji mpumbavu.
Samahani sana Ney wa Mitego kukufananisha na mfugaji mpumbavu aliyemtegea kuku wake mayai viza kisha akishangaa kwanini kuku wake atotoi.
TUONANE WIKI IJAYO SIKU KAMA YA LEO, ILA KESHO TUSINUNIANE PALE UWANJA WA TAIFA MAMBO UWANJANI