STAA WETU: THABANI SCARA KAMUSOKO: KIUNGO MSHAMBULIAJI MWENYE VITU ADIMU
Na Salum Fikiri Jr
YANGA SC imebahatika kupata mchezaji wa kulipwa mwenye hadhi ya kuitwa 'Proffesional', si mwingine ni Thabani Scara Kamusoko.
Jamaa huyu tayari ana tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba 2015 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, TFF iliamua kumpa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kikubwa na kuisaidia timu yake kukamata usukani wa ligi.
Yanga ndiyo vinara wa ligi kuu bara na leo jioni inacheza mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.
Kamusoko ametishia kiwango cha kiungo mwenzake Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, katika kikosi cha kwanza cha Yanga chini ya kocha wake Mholanzi Hans Van der Pluijm, Kamusoko amekuwa akianzia katikati huku Niyonzima akitupwa pembeni ama benchi.
Licha ya kukosekana katika mchezo wa kwanza dhidi ya Cercle de Joachim na Yanga kushinda 1-0 ugenini, leo ataonekana uwanjani na kuwaonyesha maujuzi yake.
Kamusoko anasifika kwa uchezaji wake na pia amekuwa mfungaji mzuri, mpaka sasa ana magoli matano aliyofunga kwenye mechi za ligi kuu bara, pia jumatano iliyopita aliisaidia Yanga kuingia robo fainali ya kombe la FA.
Kamusoko aliifungia Yanga bao la ushindi dhidi ya JKT Mlale ya Ruvuma katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kwenye mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-1.
Pia kiungo huyo alicheza vizuri kwenye mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga uliopigwa uwa ja wa Taifa jumamosi iliyopita, ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0 magoli yaliyofungwa na Donald Ngoma na Amissi Tambwe.
Kamusoko alizaliwa Machi 2, 1988 mjini Halale na alianza kucheza soka la ushindani kwenye timu ya Njube Sundownd kuanzia mwaka 2007 hadi 2009 alipojiunga na Underhill na mwaka 2010 alitua zake Dynamo ambayo alidumu nayo hadi 2013 alipojiunga na FC Platinum.
Mwaka 2015, Kamusoko alisajiliwa na Yanga na tayari ametokea kuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu kwenye kikosi hicho kinachowania taji la 26