KAPOMBE AWA MCHEZAJI BORA JANUARI
Beki wa pembeni wa Azam Fc Shomari Kapombe ametangazwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa mwezi Januari.
Kapombe ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda nyota wawili Jeremiah Juma Mgunda wa Prisons ya Mbeya na Miraji Adam Seleman wa Coastal Union.
Kwa maana hiyo Kapombe mchezaji wa zamani wa Polisi Morogoro na Simba Sc atajinyakulia kitita xha shilingi milioni moja.
Kapombe ambaye anacheza nafasi ya ulinzi wa pembeni, pia anamudu kucheza kiungo, kilichopelekea kuibuka mchezaji bora wa mwezi Januari kwamba aliitumikia ipasavyo Azam na kucheza karibu mechi zote tatu na kufunga magoli mawili