HAMISI KIIZA AIPELEKA SIMBA KILELENI

Na Prince Hoza, Shinyanga

Wekundu wa Msimbazi Simba Sc kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ligi kuu bara wamefanikiwa kukamata usukani wa ligi hiyo baada ya kuilaza Stand United mabao 2-1 uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Hamisi Kiiza 'Diego' raia wa Uganda amekuwa na bahati msimu huu akifanikiwa kufunga mabao yote mawili ambayo yanaiweka timu yake kileleni.
Kiiza amefunga mabao hayo kila kipindi na kumfanya afikishe magoli 16 akimuacha nyuma mpinzani waks mkuu kwenye mbio hizo Mrundi Amissi Tambwe wa Yanga mwenye mabao 14.
Stand United nao walijipatia bao la kufutia machozi lililofungwa na David Assuman.
Simba sasa iko kieleni ikiwa na pointi 45 ikiiacha nyuma Yanga yenye pointi 43 lakini ina mechi moja mkononi.
Hata hivyo Simba inaweza kupokwa uongozi na Azam Fc ambao kesho wanacheza na Coaatal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, Azam itahitaji kushinda mabao mengi ili kuipoka uongozi Simba kwani yenyewe inatambia mabao ya kufunga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA