NILIMDHIBITI DIDIER DROGBA, SEMBUSE KIIZA- BOSSOU
Na Mwandishi Wetu, Pemba
Beki wa kati wa Yanga Vincent Bossou raia wa Togo, ameshangazwa na kauli za mashabiki wa soka nchini wakishindwa kumuamini na kutamka maneno kuwa hana uwezo wa kumdhibiti mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza "Diego" raia wa Uganda.
Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye uwanja wa Gombani Pemba amedai anashangazwa na kauli hizo na amewataka eajitokeze kwa wingi wakamshuhudie atakavyomdhiboti mshambuliaji huyo anayeongoza kwa mabao.
Kiiza anaongoza kwa magoli hadi sasa ameshatupia magoli 16 akifuatiwa na mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe mwenye mabao 14.
Beki huyo amedai kuwa hsmuogopi Kiiza wala pacha wake Ibrahim Hsjibu na anawachukulia kama wachezaji wa kawaida, Bossou amewakumbushia mashabiki hao wanaombeza kuwa aliwahi kumdhibiti mchezaji bora wa Afrika Didier Drogba wa Ivory Coast.
Pia amewahi kumdhibiti mshambuliaji bora mwingine wa Afrika Mcameroon Samuel Eto'o "Fills"