NGOMA ATIMKA YANGA, KUIKOSA CERCLE DE JOACHIM JUMAMOSI
Na Ikram Khamees
Mshambuliaji wa kutumainiwa wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Donald Dombo Ngoma ataikosa mechi ya kimataifa dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa mchezaji huyo ataikosa mechi hiyo ya marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kufiwa na mdogo wake.
Ngoma amefiwa na mdogo wake jana nchini Zimbabwe akiwa uwanjani aligongana na mchezaji mwenzake na kufariki dunia, Ngoma anayekipiga Yanga ndiye baba wa familia hivyo amelazimika kusafiri kuudhuria mazishi ya mdogo wake.
Ngoma mfungaji pekee wa bao la kwanza Yanga ikiifunga Cercle de Joachim 1-0 katika uwanja wa Curepipe huko Mauritius, kukosekana kwa Ngoma ni pigo kubwa kwani mshambuliaji huyo yuko katika kiwango cha juu mno ambapo jumamosi iliyopita aliitungua Simba uwanja wa Taifa, Yanga ikishinda 2-0.
Tayari mchezaji huyo ameshasafiri kuelekea Zimbabwe, Wakati huo huo wapinzani wa Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika Cercle de Joachim wanawasili leo