SIMBA ILIVYOJIFUA JANA KAMBARAGE, STAND WAKINUSURIKA KIPIGO WAKAOMBE KWA BABU
Na Prince Hoza, Shinyanga
Wachezaji wa Simba Sc jana waliendelea na mazoezi ya nguvu katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ambapo leo jioni watachuana na wenyeji wao Stand United.
Simba inahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa ligi kuu bara na endapo itaibuka na ushindi mojs kwa moja itakwea kileleni kwa mara ya kwanza tangia kuanza kwa msimu huu.
Kocha mkuu wa Simba Jackson Mayanja anaonekana hataki mzaha awapo kazini na alikuwa akiwapigisha tizi la nguvu wachezaji wake.
bila shaka jioni ya leo Simba itachomoka na ushindi na endapo itatokea bahati mbaya Stand United ikanusurika kipigo basi wakaombe kwa babu